Sera hii ikiwekwa kuwa imewashwa hulazimisha wasifu ubadilishwe kuwa kipindi cha matumizi ya muda. Sera hii ikibainishwa kuwa sera ya Mfumo wa Uendeshaji (k.m. GPO kwenye Windows) itatumika katika kila wasifu kwenye mfumo; sera hii ikiwekwa kuwa sera ya Wingu, itatumika kwenye wasifu ulioingia ukitumia akaunti inayosimamiwa pekee.
Katika hali hii, data ya wasifu huchanganuliwa kwenye diski kwa muda wote wa kipindi cha mtumiaji. Vipengele kama vile historia ya kivinjari, viendelezi na data yake, data ya wavuti kama vile vidakuzi na hifadhidata za wavuti hazihifadhiwi baada ya kufunga kivinjari. Hata hivyo, jambo hili halimzuii mtumiaji kupakua data yoyote kwenye diski, kuhifadhi au kuchapisha kurasa.
Ikiwa mtumiaji amewasha kipengele cha kusawazisha, data hii yote itahifadhiwa katika wasifu wake wa kusawazisha kama wasifu wa kawaida. Pia hali fiche inapatikana isipozimwa kabisa na sera.
Sera ikiwekwa kuwa imezimwa au isipowekwa, kuingia katika akaunti husababisha kuwepo kwa wasifu wa kawaida.
Registry Hive | HKEY_LOCAL_MACHINE or HKEY_CURRENT_USER |
Registry Path | Software\Policies\Google\Chrome |
Value Name | ForceEphemeralProfiles |
Value Type | REG_DWORD |
Enabled Value | 1 |
Disabled Value | 0 |